HUU NDIYO UKWELI KUHUSU FREE-MASON
Niliwahi kusema kipindi cha nyuma kwamba Freemasons ina degrees thelathini na tatu, yaani kwa kifupi tunatamka 3. Hii ni namba kubwa sana kwenye ishu zao, na uzuri wa hawa jamaa huwa hawajitangazi bali unawatangaza wewe mwenyewe, yaani unawapa umaarufu, hilo ndilo jambo pekee wanalojivunia nao.
Achana na yale mabango eti Freemason wanapatikana wapi na wapi, tupigie, bro! Freemason hawaweki matangazo popote pale, wewe mwenyewe tu unawajua na kuwatangaza. Mfano lile kanisa lao pale Posta, mbona hawakuwahi kusema tuna kanisa mahali fulani ila ghafla tu umelijua, halafu unawaambia wenzako na wenzako, mwisho mnawajua na kuwatangaza.
Ukienda kwa Mafreemason watakwambia kazi zao ni kusaidia jamii, na ni kweli wanasaidia jamii. Hawa majamaa wanajenga sana mahospitali, shule, vituo vya watoto yatima na vingine vingi tu na ndiyo maana niliwahi kuwaambia huko nyuma kwamba kama unataka kuwa Freemason kitu cha kwanza uwe na pesa, hawachukui masikini kwa sababu wao wanataka kuisaidia jamii.
Alama ya Freemason na wenzao Illuminate huwa ni nyoka na pembetatu. Kwa nini nyoka? Kwanza ukisoma Biblia, kwenye stori ya Musa baada ya kurudi mlimani na kukuta watu wanaabudu miungu, akatengeneza nyoka wa shaba, akawaambia kwa kila mtu atakayemwangalia yule nyoka basi atapata uponyaji, na ikawa hivyo.
So wao wakaamua kuichukua alama ya nyoka kumaanisha uponyaji. Ukienda kwenye mahospitali yao unakutana na alama za nyoka, angalia hata taasisi zingine za kidini, kuanzia majengo, mavazi na mengine unakutana na alama ya nyoka.
Na majengo mengi makubwa yana ishara fulani za nyoka, either macho ama magamba. Hata ukiangalia magari mengine yalivyo kwa mbele, yanaonekana kama nyoka. Just Google utayaona.
Subiri kwanza! Kunywa maji.
Ukiwauliza wao, wanakupiga saundi kwa staili hiyo ila ukweli unakuwa ni mmoja tu, inatumika alama ya nyoka kwa sababu ndilo umbo la kwanza kabisa ambalo shetani alijionyesha kwa binadamu katika bustani ya Eden.
Kwao, nyoka anaonyesha nguvu kubwa ya kumshawishi binadamu kama alivyoshawishiwa Hawa, nyoka kwao anaonekana kuwa na busara. Hata Biblia iliandika kwamba yule nyoka alikuwa na busara, so wanapotumia alama ya nyoka humaanisha hayo yote.
Wanatumia pembetatu. Hujiulizi kwa nini sio pembenne? Ama pembetano? Nilikwambia kwamba wao wana degrees 33, hapo kuna tatu tatu mbili na ndiyo maana wanaitumia sana namba tatu.
Angalia alama zao za vidole wanavyoweka akina Jay Z, wanakuwekea pembetatu. Hii ni namba yenye nguvu sana ambapo ukitoka namba hiyo, inayofuata ambayo pia kwao wanaipa kipaumbele ni namba 6. Kutakuwa na namba 666 ya mpinga Kristo.
Na alama ya tatu ambayo nilitaka niisahau ni jicho. Wanatumia sana jicho kama alama nyingine. Kwa nini jicho? Hakuna dhambi duniani inayofanywa bila kuonwa. Kwanza kitu cha kwanza unaona na ndiyo unafanya dhambi.
Unamuona dada mzuri, unamtongoza, unalala naye. Unakwenda baa kunywa soda, ukifika pale unashawishiwa na pombe unayoiona, unainywa. Kila dhambi inayofanyika, kwanza huonwa. Kwa maana hiyo jicho huwa kitu cha kwanza kabisa kinachompelekea mtu kufanya dhambi.
Unamchukia mtu baada ya kumuona, either picha yake ama kukutana naye. So wanapotumia alama ya jicho huwa wanamaana kubwa, kwamba hicho ndicho msingi wa kila kitu. Ili Hawa akubaliane na nyoka, kwanza akamuona, wakazungumza.
Kitu ambacho hakionekani kwa macho ya binadamu huwa kinakuwa kimejazwa mashaka sana, binadamu anachokitaka kwanza ni nguvu ya macho kukiona. Unamuabudu Mungu, kwanza unatakiwa kumuona. Kule Asia wameamua kujitengenezea miungu yao kwa fundi seremala, wanaiabudu, wanaiona. Ukibishana nao wanakwambia tuonyeshe Mungu wako.
So wanatumia vitu vitatu. Pembetatu, jicho na nyoka. Na niliwahi kukwambia kwamba huu ulimwengu upo chini yao. Chukua dola moja, iangalie. Pale unaiona kabisa alama ya pembetatu na jicho. Unabisha? Hebu iangalie hii dola moja kwa pembeni. Hii inamaanisha nini? Pesa zote duniani zinatengenezwa na hawa majamaa, si unajua hata benki ya dunia ipo chini yao?
Kuna kasauti tu moyoni kananiambia kitu halafu napotezea kasije kunigombanisha na watu. Eti kananiuliza mbona hata ile 500 ya noti ilikuwa na nyoka....
Jamani eeeeeh! Asubuhi njema.


