YALIYOMO KWENYE NEMBO HII INAYO TUMIWA NA FREE-MASON

Pale mjini Masonic, hii ndiyo huwa logo yao lakini swali moja tu limekuwa likiulizwa, hiyo G humaanisha nini? Je, humaanisha God ama nini? Wengi wao hawajui. Ngoja nikufafanulie kidogo mtu wangu wa nguvu.


Au subiri kwanza! Acha nikufafanulie logo nzima ili siku nyingine usije kuniuliza maswali.


Hapo unaona Square na Compass. Hiyo inasimama kumwambia memba kusimama kwenye mipaka ama kuwa na mipaka. Yaani NIDHAMU. 


Braza wewe unajiona kuwa na nidhamu lakini nikwambie tu hauna nidhamu kama hawa majamaa. Hawa wana nidhamu kwenye kila kitu, kuhusu maisha yao mpaka matumizi yao ya pesa. 


Freemason hamwagi pesa hovyo, wamefundishwa nidhamu kwenye kila kitu. Wanaiheshimu pesa kwa sababu usipokuwa na nidhamu kwenye mambo ya pesa, unakuwa umekwenda kinyume na katiba yao.


Kila anachokifanya kiwe kwenye vipimo na midhani ya FREEMASON. So memba hujiangalia hapo mienendo matendo hadi namna ya kuamua.


Okay! Turudi kwenye herufi G. Kama wewe hujui maana ya hii herufi haupo peke yako, unaweza kuwa na digrii zote 33 lakini bado usijue hii G inamaanisha nini. Usishangae! Nakwambia kitu halisi kabisa.


G kwa Kiebrania ina thamani ya 3, kumbuka Kiebrania ina herufi 22 tu. Sasa 3 ni ni force 3 zinazoitawala ulimwengu. Hebu niwarudishe kwenye somo la jana, nilisema kuna digrii tatu, si ndiyo, halafu ndani ya hizo digrii kuna digrii kadhaa (Pitia somo la jana) sasa ule mgongo kabisa wa digrii 3 ndiyo umechukuliwa na kuwekwa hiyo G kwa sababu ni herufi ya tatu kwenye mtiririko wa herufi za Kiebrania.


Sijui mnanielewa ama nimewaacha. Acha tuendelee, ukiirudia ya jana utaelewa.


Sasa G inamaanisha nini? G hii imanaanisha Gnosis. Hili ni neno la Kigiriki lenye maana ya Knowledge kwa Kiingereza na maarifa kwa Kiswahili.


Hapa acha nikwambie kitu. Wengine wameifafanua G kama Great ama God ama Grant kwa maana ya cheo kikubwa sana.


Sasa pale Freemason kuna kiongozi wao kwenye kuabudu. Hapo nisikilize. Kitu cha kwanza ni kukukumbusha kwamba hawa washikaji wanaijua sana dunia, wamesoma na wana utambuzi mkubwa sana.


Wao wanakuona wewe huabudu kama inavyotakiwa kanisani kwako ama msikitini na ndiyo maana Freemason hawachagui dini, hata imamu unaweza kuungana nao na kisha kuabudu katika kanisa lao. Nisiingie sana huko nitakuboa.


Sasa yule kiongozi anayeongoza ibada zao huitwa Worshipful Master. Huyu mtu huchaguliwa na wanachama wake, ikitokea akafa, basi wanamchagua mwingine na mambo yanaendelea.


Huyu kiongozi huchaguliwa kila mwaka, yaani unaweza kuongoza mwaka huu na mwaka ujao akawa mwingine ama ukaendelea wewe. Na kila wanapokuwa kanisani kuabudu, ni yeye tu ndiye ambaye huruhusiwa kuvaa kofia. Sio kofia kama yako, kuna kofia zao maalumu wanazozivaa. 


Freemason wameweka sheria zao kwamba vazi kubwa huwa ni suti nyeusi. Huwezi kumuona Freemason akivaa suti za rangi nyingine mara kwa mara. Kwao, ule weusi unamaana kubwa sana.


Hebu subiri! Nikuulize kitu? Ushawahi kujiuliza kwa nini kwenye harusi watu hupendelea kuvaa suti nyeusi? Ushawahi kujiuliza kwa nini kwenye mahakama nyingi duniani mahakimu huvaa majoho meusi? Ushajiuliza kwa nini polisi wa Marekani wengine huvaa sare nyeusi? Ushajiuliza kwa nini Usalama wa Taifa wengi duniani huvaa nguo nyeusi?


Bro! Nikwambie jambo moja tu, Freemason wameishikilia hii dunia na wanafanya kile wanachokitaka wao. Wao wana serikali zao, wanaamua nini kiwe sare na nini kipuuziwe. Wao wanaiendesha dunia hii kwa miaka mingi na wameanzisha vitu ambavyo tunavichukulia kama kawaida ila ni kuwakilisha kile wanachokifanya.


Freemason wanafanya mambo ambayo wewe huwezi kujua yana nguvu kiasi gani. Kuna alama za vidole ukiweka zinakufanya ujiamini muda wote, zina nguvu sana, sema sisi hatujui kwa kuwa hatuna elimu.


Waangalie mastaa duniani wakiwa wanahojiwa, angalia vidole vyao huwekaje! Aina ile ya uwekaji wa vidole huwa na nguvu sana, hufanya mtu ajiamini. Wao ndiyo waliosema hata mtu anapooa anatakiwa kuvalishwa pete kidole cha pili kutoka kidole kidogo. Kwa nini? 


Ni kwa sababu kidole hicho kina mshipa ambao huenda moja kwa moja kwenye moyo. Kwa maana hiyo mtu anayekuvisha pete anakuwa ameweka kitu moyoni mwako. Hujajiuliza kwa nini wakati wa harusi ni kidole kimoja tu ndiyo huvishwa pete?


Bro! Haya huyajui! Washikaji wana elimu kubwa sana. Mikutano yote ya Freemason hufanyika saa tatu. Iwe ni asubuhi ama usiku, ila iwe saa tatu usiku. Kwa nini saa tatu? Kwani jana nilimwambia digrii zao zipo ngapi? Zile za kwanza zipo 3 ambapo ndani yake zipo nyingi mpaka 33 ambazo ni za mwisho. Pingili za uti wa mgongo zipo 33. Hivyo wao wamechukua namba 3 kama alama yao muhimu sana.


Braza cheki saa yako! Ina moja mpaka 12, si ndiyo? Hapo kila muda kwa Freemason wana maana yao, yaani kuanzia 1, wanafanya hiki, 2, wanafanya hiki mpaka hiyo 12. Unataka kujua wanafanya nini kwenye hizo saa? Tusbiri App ianze kazi.


Leo nimekudokeza hiyo saa 3 kwamba ni muda wao wa kupiga mvinyo na kuweka vikao, ila hayo masaa mengine kuna mengine mengi huyafanya. Ni nini? Tusubiri App manake mengine ni uhuru sana kuyaandikia huko.


Cha msingi jua tu kwenye kila kitu unachokifanya, Freemason wamekishikilia vilivyo. Utakwenda kanisani, utaabudu, misikiti tutaswali, ila jua kwenye kila kitu tunachokifanya tunafanya kile walichotaka kukifanya.


Unashangaa! Hujui hili?


Ushajiuliza kwa nini unakwenda kuswali msikitini alfajiri? Saa saba kasoro? Saa kumi? Yaani kwa nini swala ni tano na si saba ama kumi? Kwa nini masaa ni hayo ndiyo unakwenda msikitini? Kwa nini kanisani una misa kadhaa? Kwa nini wanakutaka usali ama kuswali zaidi ya mara moja Ijumaa ama kanisani?


Freemason ilikuwepo kabla ya Ukristo na kabla ya Uislamu. Walikuwa wakifanya yao kwa siri kubwa mpaka pale sasa walipojiweka wazi June 24 mwaka 1717. Yaani wakakifanya official na watu wakifahamu, ila kilikuwepo miaka mingi sana huko nyuma.



Bro...Bro...Bro...Nikwambie tu kwamba kila kitu kipo chini ya kontrol yao, kiaje? Tusubiri GREEN HACKER AZIDI KUZAMA MAPANGONI MWAO.


MWISHO.

نموذج الاتصال