Kama unataka kutengeneza bot lako la muziki Telegram bila mambo mengi nimekusogezea mchongo mzima hapa. Hautahitaji kuwa profesa wa kodi, unahitaji tu simu yako au PC na dakika chache.
Hizi hapa ndio hatua za kufuata:
Ukishindwa nitumie ujumbe kwenye hii website kisha GREENHACKER 😈 nikusaidie
1. Pata "Token" kutoka kwa BotFather
Huyu ndio baba lao Telegram. Bila yeye hupati bot.
Mtafute `@BotFather` kwenye Telegram.
Gusa `/start` kisha tuma command ya `/newbot`.
Mpe jina bot lako (mfano: Bongo Music Bot.
Mpe username (lazima iishe na `_bot`, mfano: `my_track_bot`).
BotFather atakupa API Token Icopy hiyo, itunze kama siri ya moyo wako.
2. Tafuta "Host" (Sehemu ya kulilaza bot)
Bot haliwezi kufanya kazi hewani tu, linahitaji sehemu ya kukaa (Server). Kwa kuanzia, tumia hizi njia rahisi:
Heroku au Railway.app: Hizi ni platform nzuri kwa ajili ya kurusha bot lako.
Replit: Hii ni nzuri sana kama unataka kuandika kodi kidogo na ku-run bot papo hapo.
3. Tumia "Ready-Made" Scripts (Njia ya mkato)
Badala ya kuandika kodi kuanzia mwanzo, unaweza kutumia kodi ambazo watu washatengeneza (Open Source).
Nenda GitHub na utafute "Telegram Music Bot Python".
Miradi maarufu ni kama Yukki Music Bot au VCPlayerBot
Copy hiyo kodi (Clone) kwenda kwenye server yako (Replit au Heroku).
4. Unganisha na API ya Muziki
Weka hizi details kwenye file la `.env` au `config` ya bot lako pamoja na ile Token ya BotFather.
5. Washa Mashine
Kama unatumia Replit, bonyeza Run
Kama unatumia Terminal, piga command ya `python3 main.py`
Bot likiwa "Online", nenda Telegram, li-add kwenye group, lipige kiredio (Admin rights), na uanze ku-request nyimbo kwa `/play [jina la wimbo]`.
Zingatia: Kutengeneza bot la muziki linalopiga sauti kwenye Voice Chat ni gumu kidogo kuliko lile la kutuma ma-file ya mp3. Kama unataka lile la kutuma file tu, hiyo ni sekunde chache
