Ukweli wa Kushtua Kuhusu Pegasus – VIRUS Anayeishi Kwenye Simu Yako
![]() |
| GREEN HACKER 😈 |
Je, unajua kuwa kuna software inayoitwa Pegasus virus ana uwezo mkubwa ambayo inaweza kusoma meseji zako za WhatsApp, kufungua kamera*, kusikiliza mazungumzo kupitia mic
Pegasus si virusi vya kawaida. Ni spyware hatari iliyoundwa na kampuni ya NSO Group kutoka Israel, kwa lengo la kusaidia serikali kupambana na ugaidi. Lakini baadae, iligundulika kuwa ilitumiwa kufuatilia waandishi wa habari, wanaharakati, wanasiasa na hata watu wa kawaida
Nini kinafanya Pegasus kuwa ya kipekee?
- Huhitaji kubofya link yoyote (zero-click exploit)
- Inaweza kuingia kupitia WhatsApp, iMessage, au hata missed call tu
- Haionekani kirahisi hata na antivirus
- Mara nyingi inaondoka yenyewe baada ya kutekeleza kazi
Kwa kifupi, simu yako inaweza kuwa “jicho” la mtu mwingine — anayeona, anayeandika, na anayesikiliza maisha yako yote bila ujuzi wako.
Cha kushangaza zaidi: Pegasus imeweza kudukua simu za viongozi wakuu wa nchi, watu mashuhuri duniani, na mamilioni ya raia — kwa siri
Ripoti za Amnesty International na mashirika ya kimataifa kama Citizen Lab zimebaini Pegasus ilitumika kudukua:
- Waandishi wa habari mashuhuri
- Viongozi wa upinzani
- Wanasheria wa haki za binadamu
- Wanaharakati wanaopinga serikali
- Viongozi wa dini na hata marafiki wa walengwa
Wakati mwingine, watu walikuwa wanauawa muda mfupi baada ya simu zao kufuatiliwa.
Kwa Nini Hii Ni Hatari Sana?
Pegasus haionekani na antivirus za kawaida. Mara nyingi ikimaliza kazi yake, hufuta ushahidi wa kuwepo kwake. Ndiyo maana hata wajuzi wa teknolojia wameshindwa kuigundua mapema.
Aidha, ni ghali mno — leseni moja ya kutumia Pegasus kwa kudukua hadi watu 10 inaweza kugharimu zaidi ya USD 500,000* (zaidi ya Tsh Milioni 1,200). Hii inaonyesha kwamba haikuundwa kwa watumiaji wa kawaida — bali kwa mashirika makubwa na serikali.
Je, Unaweza Kujilinda?
Hakuna njia ya uhakika ya kujilinda 100%, lakini unaweza:
- Tumia *Signal kwa mawasiliano nyeti
- Epuka kutumia WhatsApp au iMessage kwa taarifa binafsi
- Weka simu yako updated kila mara
- Tumia VPN unapotumia intaneti ya umma
- Usibofye link usiyoijua au ya kutia shaka
- Zima simu yako mara moja moja (reboot inasaidia kusafisha RAM na apps za siri)
©2025 copyright under authority of IT TECHBROSS GROUP written by GREENHACKER
MWISHO UNAWEZA ACHILIA COMMENT YAKO HAPO CHINI 👇

.jpeg)
.jpeg)