Netflix anapiga sana pesa, tena sana aiseee! Wiki hii amepiga bonge moja la dili na Warner Bros, yaani ametoa kiasi kikubwa mno cha pesa.
Ni dola bilioni 82.7 ameinunua kampuni hiyo ya filamu ambayo ndani yake kuna makampuni mengine mengi, yaani kwa sasa Netflix amechukua haki miliki za filamu zinazozalishwa humo.
Dola bilioni 82.7, wazee msichukulie poa hizi pesa, ni nyingi mno mno mno.
Hii inamaanisha nini?
Netflix now anaumiliki ulimwengu wa DC, yaani anazimiliki filamu zote za Super-Man, Batman, Wonder Woman, Flash na charasters wengine kutoka kwenye ulimwengu wa DC. Kwa maana hiyo filamu hizo zitakwenda kuwa chini ya Netflix.
So hapa wataamua, kama Super-Man atatoa filamu, wanaweza kuiweka moja kwa moja Netflix ama waipeleke kwanza kwenye jumba la sinema, wao wataamua nini cha kufanya.
Kuna ile channel ya katuni ya Cartoon Network ambayo ilitulea, ile sasa itakuwa chini yao.
Netflix imezichukua filamu zote za Harry Potter mpaka zile ambazo zitakuja kutolewa baada ya hapo.
Kuna ile shoo ipendwayo sana ya FRIENDS, nayo ipo chini yao.
Pia imeichukua shoo ya Game of Thrones, kuanzia yenyewe mpaka Spin-off zake kwa kuwa hata Ho ipo chini yao.
So Netflix imechikua studio zinazotengeneza filamu na shoo hizo kama HBO Max na HBO.
Kama kuna series ambayo ilikuwa chini ya HBO ikiwemo Breaking Bad, kwa sasa zote zipo chini ya Netflix. Yaani wametoa pesa nyingi sana na wataingiza pesa nyingi zaidi.
Kumbuka kwa mwaka Netflix inaingiza dola bilioni 42.7, hapo tutoe sisi ambao tunaangalia muvi zao bila kulipia popote pale.
Yaani kwa kifupi ni kwamba Netflix inakwenda kuwa na thamani ya juu mara 100 ya iliyonayo kwa sasa.
unaweza uka achilia comment yako moja kwa moja apo chini kuhusu ukweli huu ulio andikwa na bwana Greenhacker ama Directorkessy

