Mbinu Sahihi za kutumia AI
Eleza Kwanza, Uliza Swali Mwisho
Hatua 1: Weka Muktadha (Context)
Eleza hali yako ilivyo sasa.
“Mimi ni kijana wa Tanzania, nina simu tu, sina mtaji mkubwa, na nataka kuanza biashara mtandaoni.”
Hatua 2: Eleza Tatizo au Changamoto
AI lazima ijue unakwama wapi.
“Changamoto yangu ni sijui ni biashara ipi inaweza kunifaa kwa mazingira yangu na ujuzi nilionao.”
Hatua 3: Eleza Unachohitaji Itatueje
Eleza matokeo unayotaka na jinsi ya kuyapima.
“Nahitaji unipendekezee biashara 3 zinazowezekana, uzieleze kwa hatua za kuanza, gharama zake, na makosa ya kuepuka.”
Hatua 4: Uliza Swali Lililoelekezwa
Uliza swali la uamuzi.
“Ni biashara ipi kati ya hizo itanifaa zaidi nikizingatia hali yangu, na kwa nini?”
Mfano Kamili wa Prompt Bora
“Mimi ni kijana wa Tanzania mwenye simu ya Android, nina intaneti ya kawaida, na nina maarifa ya msingi ya mitandao ya kijamii. Nataka kuanza kujitengenezea kipato cha mtandaoni bila mtaji mkubwa. Changamoto yangu ni kutojua ni njia ipi itaniingizia pesa kwa haraka na kwa uhalisia wa mazingira ya Tanzania. Nisaidie kwa kunipatia njia 3 zinazowezekana, eleza hatua za kuanza kila moja, muda wa kuona matokeo, na makosa yanayowafanya watu wengi washindwe. Baada ya hapo, nichagulie njia moja iliyo bora zaidi kwa hali yangu na nieleze kwa nini.”

