Machapisho

Huduma ya tick tock Tanzania ya sitishwa rasmi

HUDUMA YA TIKTOK LIVE YASITISHWA TANZANIA, WATUMIAJI WATAKA MAELEZO RASMI.

 

Watumiaji wa mtandao maarufu wa TikTok Nchini Tanzania, hasa wale wanaotumia TikTok LIVE kujipatia kipato, wamekumbwa na hali ya sintofahamu baada ya huduma hiyo kushindwa kufanya kazi kama kawaida.

 

Kwa sasa, TikTok LIVE haipatikani bila kutumia VPN, jambo ambalo limewafanya baadhi ya Watumiaji kuhisi kuwa huenda huduma hiyo imefungwa au kuzuiwa kimya kimya na mamlaka husika.

 

Ingawa bado hakujatolewa taarifa rasmi kutoka serikalini kuhusu hatua hiyo, hali inavyoendelea imezua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya Watumiaji wakiomba TCRA au Wizara ya Habari na Mawasiliano kutoa tamko rasmi.

 

“Kwa sasa lazima uwashie VPN ili upate TikTok LIVE. Bila hiyo, huwezi kuingia live, wala kuona waliopo live,” alisema mmoja wa Watumiaji wa TikTok kupitia ukurasa wake.

 

Watumiaji wengi wa TikTok Tanzania wamekuwa wakitumia LIVE si tu kwa burudani, bali pia kama chanzo cha kipato kupitia zawadi za kidijitali kutoka kwa Wafuasi wao. Kusitishwa kwa huduma hiyo ni pigo kubwa kwa Vijana wengi waliotegemea mtandao huo kuendesha maisha yao.

 

Mpaka sasa, bado haijafahamika ni nini hasa sababu ya kusitishwa kwa huduma hiyo, na iwapo ni suala la muda au hatua ya kudumu.

 

Toa maoni yako 

#GREEN HACKER 👿

#IT TECH BROSS GROUP 

#TikTokLIVE #TCRA #TanzaniaDigital #HabariZaMitandaoni #MitandaoYaKijamii

Getting Info...

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.