المشاركات
Facebook inakuingiziaje pesa na vigezo vyake ni vipi
FACEBOOK INAKUINGIZIA PESA VIPI? NI VIGEZO VIPI INATAKIWA UTIMIZE ILI UANZE KULIPWA? NA JE NI VITU GANI NI MUHIMU VYA KUWA NAVYO KABLA HUJATUMA OMBI?
Twende Pamoja... 🚀
Facebook Inawalipa Content Creators wanaoweka Video katika Platform yao kwa Kupachika Matangazo (Ads) katika Video hizo kama Ilivyo kwa YouTube inayosimamiwa na Google. Facebook Wanalipa Content Creators pekee na sio Business Pages. Wanalipa Profiles zilizo katika Professional Mode na Official Pages sio Meme Pages/Account, Fan Page au Meme Profiles.
Je ni Vigezo gani Ukiwa navyo Utajua Page au Profile yako Iko tayari kwaajiri ya Kulipwa?
VIGEZO:
• Uwe na Original Content, yaani Content zisizo na Copyright, Content ulizotengeneza Mwenyewe bila Kutumia idea ya Mtu
• Video zako ziwe na Jumla ya Minutes Viewers 600,000 kwa Siku 90 Zilizopita (Download Creator Studio App) kuona Data hizi
• Uwe Unaishi katika Nchi Facebook inaposupport Monetization, Mfano wa Nchi ni Switzerland, Canada, USA, UK, South Africa, India, United Arab Emirates (UAE), German, China, Indonesia, Norway, na Ikiwa Hauishi Katika Nchi hizi Waweza Kutumia VPN kwa Siku 15 kabla ya Kutuma Ombi ili KuAccess feature hii
• Page / Profile yako Iwe na Jumla ya Followers 10,000 (10K) au Zaidi
• Uwe Umepost Video 3 au Zaidi kwa Siku 30 zilizopita
• Uwe Haujawahi Kuvunja Sheria za Facebook
• Page yako iwe na Tittle za Individuals, Influencers au Public Figures mfano. Model, Author, Artist, Video Creator, Digital Creator, Blogger NK. na Ikiwa ni Profile basi iwe katika Professional Mode, Mfano wa Professional Mode ni kama Account hii
• Lazima Uwe na Business Account ili KuAccess Feature hii
• Lazima Uwe na Laptop au Computer ili KuAccess feature hii
• Account yako Iwe Active bila Restrictions zozote.
VITU MUHIMU VYA KUWA NAVYO KABLA HUJATUMA OMBI
• Uwe na Passport/Kitambulisho cha Taifa (sio Namba)
• Uwe na VAT
• Uwe na TIN number (Leseni ya Biashara
• Uwe na Link ya Page yako Kichwani
• Uwe na Laptop/Computer (Sio Lazima kama Utaunganishiwa)
• Uwe na Card ya Bank au Paypal Account
• Uwe na Facebook ID ya Page/Profile yako (Kupata Facebook ID ingia www.facebook.com nenda kwenye Profile yako Utaona ID yako)
• Ni Muhimu kuangalia Kwanza Ikiwa Umekidhi vigezo (ingia www.business.facebook.com/creatorstudio au Download Creator Studio kutoka Google Play au Appstore na Weka Taarifa zako)
• VAT na Tin Number Ni Muhimu katika Zoezi hili, Unaruhusiwa Kutumia VAT au Tin ya Mwingine (ila Hakikisha Majina yanafanana na Business Account yako)
-----
Maelezo ya Video Nitatoa Wakati Mwingine hapa Hapa kwa Upana zaidi. Stay Safe, Tuko hapa Kusaidiana!!
Getting Info...
