Umeshawahi Kutumiwa Link ya kupata GB za Bure?
Kuna tabia imeenea Sasahivi kila Mahali naona iko On Fire na Kila mtu anafanya kwa kuwatumia watu kadhaa kwa idadi alio ahidiwa ikifikia ndio atapewa hizo Gb wanazohisi wangepewa mara tu baada ya kutumia watu link..
Hii ni Hatari sana Maana Siku zote usikubari kufungua Link ambayo Haina Domain Name ya Kampuni Husika yaani Kwa mfano (https://Tigo.com) mara nying Link zao huwaga hazina Domain wala Identity ya kuashiria kuwa ni Offer za ukweli na Sio Upigaji...
Mfano wa Links zao Huwaga Hivi
Vodacom
https://just.get-data.buzz/40GB
Airtel
https://just.get-data.buzz/40GB
SafariCom
https://just.get-data.buzz/40GB
Telkom
https://just.get-data.buzz/40GB
Tigo
https://just.get-data.buzz/40GB
⚠️NOTE: usitumie Hizo link kufanya Makosa nilio ongelea na ukatuma tena kwa Watu "just for educational Purposes Only"
mAdHara GAni yAnawEza kutOkeA?
✅1: KEY LOGGING ATTACK
✅2: PHISSHING ATTACK
1:KeyLogging
• baadhi ya link zinaweza kuwa ni direct link za kudownload apk file mara tu baada ya kugusa link na baada ya hapo Zina ji install zenyewe na huwezi kuziona kwenye Simu yako,KeyLogger ni aina ya Malicious Program ambayo inakuwa designed ili kutrack na ku Record kila Kitufe utakacho bonyeza kwenye Keyboard yako ya Simu au Computer.
• Hii inamaana kuwa inaweza kuCapture/kukamata Sensitive information & taarifa muhimu kwa mfano Passwords,Usernames,Credit Cardnumbers, au hata data nyinginezo za Kibinafsi mara tu unapokuwa unaaandika kwenye Keyboard ya Simu yako.
• KeyLoggers inaweza kuji install yenyewe kwenye Simu ya mtumiaji Bila hata ruhusa yake na zinaweza kufanya kazi kimya kimya kwenye background,taarifa zako zikishakuwa Captured/zimekamatwa huwaga zinatumwa kwenye remote location ambako CyberCriminals(waalifu wa mtandao) wanaweza kuzipata immediately na utakuwa hatarini kuwa HACKED
2: Phishing Attack
• Hii ni aina ya Cyber Attack ambako CyberCriminal/mhalifu anatumia mbinu za udanganyifu na ulaghai ili kupata sensitive Information/taarifa za siri za mtumiaji kama vile Passwords,Bank CardNumbers na baadhi ya taarifa zinazoweza kuwa muhimu.
• Kwenye Phishing Attack hapa CyberCriminal anaweza kujifanya yeye ni taasisi au kampuni inayojulikana kama vile Benki,Kampuni ya mtandao,au shirika la serikali na huwaga wanatuma Fake Emails au mda mwingine huwaga wanatuma fake Website ambazo ukiziangalia huwa zinafanana na zile Original,Hizi Emails na Websites zinaweza kuwekwa Link ambayo mara itakapo bonyezwa itapelekea kumuomba mtumiaji aingize taarifa zake za Siri.
• Mara tu Mtumiaji atakapo ingiza taarifa zake za Siri kwenye hizo Fake Websites,Cyber atazikamata taarifa hizo kwa madhumuni mabaya kwa mfano kuiba pesa kwenye account ya Benki au hata utapeli wa kimtandao
Cha kuzingatia ni kuzipuuza tu hizo links na kutozifungua kwakuwa ushajua madhara yake sasa
𝐦𝐰𝐚𝐧𝐝𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐠𝐨𝐨𝐠𝐥𝐞 𝐭𝐲𝐩𝐢𝐧𝐠
*_react_*
Tags
Special tricks
